Wagonjwa katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Kenyatta wanaathirika na mgomo wa madaktari

  • | Citizen TV
    322 views

    Mgomo wa wahudumu wa afya pamoja na wafanyikazi wengine wa hospitali ya rufaa ya chuo kikuu cha Kenyatta umeingia siku ya pili. Wanaogoma wakilalamikia uongozi mbaya na mazingira duni ya afya hospitalini humo ila wagonjwa ndio wanaathirika zaidi. Imewalazimu baadhi yao kuanza kuhamia hospitali nyengine hususan wale wanaohitaji matibabu muhimu kama vile ya ugonjwa wa saratani na upasuaji.