Watu 127, wengi wao raia wauwawa Sudan, Jumatatu na Jumanne

  • | VOA Swahili
    470 views
    Siku ya Jumanne (Desemba 10), Vikosi vya Rapid Support Forces - RSF, vilishambulia kwa mizinga mizito katika eneo linalodhibitiwa na jeshi huko Omdurman, sehemu ya jimbo la Khartoum, kulingana na wakazi. Mawakili wa dharura walisema siyo chini ya watu 20 waliuwawa, wakiwemo angalau watu 14 ambao walikuwa ndani ya basi ambao lilipigwa. Serikali ya jimbo hilo, inayodhibitiwa na jeshi, ilisema watu 65 walikuwa wameuwawa, na majeruhi wengine kadhaa walihamishiwa katika hospitali ya karibu ya Al-Naw. Miili iliyohifadhiwa katika mifuko iliwasili hospitali wakati waliojeruhiwa walikaguliwa na gavana wa Khartoum Ahmed Osman Hamza. Wanaharakati wa kutetea haki walisema takriban watu 127, wengi wao raia, wameuwawa nchini Sudan Jumatatu na Jumanne kutokana na mapipa ya mabomu na mashambulizi ya makombora kutoka pande zote zinazopigana. Miezi 20 ya vita kati ya jeshi na wanajeshi wa Rapid Support Forces RSF vinageuka na kuongezeka kwa umwagaji damu wakati juhudi za kusitisha vita zimekwama, na migogoro kwingineko imetawala mtizamo wa dunia. - Reuters #sudan #omdurman #vita #raia #rsf #wapiganaji #jeshi #khartoum #jimbo #vifo #voa #voaswahili