Mchekeshaji maarufu afafanua kuwa Usanii na Uaskofu wake, havina mgongano

  • | VOA Swahili
    432 views
    Mchekeshaji maarufu kutoka nchini Tanzania, Askofu Emmanuel Mgaya wa Kanisa la Free Church Tanzania, al-maarufu kama Massanja Mkandamizaji, amefanya ziara nchini Marekani kwa mwaliko wa taasisi ya Ambassadors for Childrens Health. Taasisi hii inafanya tamasha la kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Watoto nchini Tanzania na amezungumza na Sunday Shomari ambaye kwanza alitaka kujua mchekeshaji huyu maarufu anatimiza vipi majukumu ya kanisa na biashara ya uchekeshaji. #massanjamkandamizaji #mchekeshaji #askofu #emmanuelmgaya #tanzania #thecomedy #voa #voaswahili