Iwe mvua au jua, huko Luanda viatu lazima viwe vinang’ara

  • | VOA Swahili
    485 views
    Je ni utamaduni, au kawaida, au ni tabia? Kwa sababu yoyote ile, wananchi wa Angola wana desturi ya kuhakikisha viatu vyao vinang’ara kila asubuhi. Wavulana kama Tonilson wanapata kipato chao kwa kusafisha na kung’arisha viatu vya wateja wao. Kwa kwanza 200, Tonilson anang’arisha viatu kwa haraka kama mtu asiyekuwa na muda wa kupoteza wakati.Haachi kitu chochote, si mchoyo wa kutumia povu au dawa ya viatu. Nilipomwambia yeye ni kijana mwepesi zaidi katika jukumu hili, alitabasamu na kugeuza uso wake. Pengine kwa sababu kupongezwa hakutamzuia asipate njaa au kwasababu kanda za video kama hiyo bado hazijabadilisha maisha yake. @mayradelassalette #luanda #angola #shoeshine #wateja #tonilson #viatu #kungarisha #voa #voaswahili