Inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja adai polisi hawateki nyara wakenya

  • | Citizen TV
    1,364 views

    Inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja ameendelea kukana kuwa maafisa wa polisi wanahusika na visa vya utekaji nya wa wakenya, haswa kuhusiana na kutoweka kwa vijana watatu wiki hii. Kanja kwenye mahojiano ya kipekee na runinga ya Citizen pia ameendelea kukanusha mauwaji ya wachimba dhahabu katika eneo la Hillo kaunti ya Marsabit ambako watu watatu waliripotiwa kufariki hivi majuzi. Seth Olale alizungumza naye awali na kutuandalia taarifa hii