Viongozi wa kidini waikosoa serikali ya Ruto kwa kuteka nyara vijana wa Kenya

  • | Citizen TV
    2,213 views

    Wakristo nchini waliungana na wenzao duniani kuadhimisha sikukuu ya krismasi huku viongozi wa makanisa wakichukua fursa kukosoa serikali kwa visa vya utekaji nyara wa vijana. Viongozi wakuu wa makanisa ya kikatoliki na kianglikana nchini kwenye hotuba zao wameitaka serikali kusitisha mara moja visa vya utekaji nyara wanapokosolewa. Mary Muoki anaarifu kuhusu visa vya utekaji nyara vilivyowagusa viongozi wa kidini siku hii ya krismasi