Uharibifu wa wanajeshi kutoka Somalia kijijini Ishakani, Lamu

  • | Citizen TV
    26,277 views

    Kijiji cha Ishakani huko Lamu kilihifadhi wanajeshi zaidi ya 900 kutoka Somalia waliokimbilia humu nchini baada ya mapigano kati ya Wanajeshi wa Jubaland na wale wa Somalia National Army majuma mawili yaliyopita. Wakazi wa kijiji cha Ishakan sasa wanalalamikia uharibifu mkubwa wa miundo msingi kama vile shule na vyoo kando uliotokana na kuhifadhiwa kwa wanajeshi hao eneo hilo. Na kama anavyoarifu Abdulrahman Hassan, wakazi hao sasa pia wanakabiliwa na mlipuko wa maradhi ya Kipindupindu.