Uongozi wa Jimmy Carter ulikumbwa na changamoto zipi?

  • | BBC Swahili
    310 views
    Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter alikuwa kiongozi mwenye umri mkubwa zaidi nchini humo. Carter aliongoza muhula mmoja madarakani kuanzia 1977 hadi 1981. Wakati wa uongozi wake kama rais alikabiliwa na changamoto za sera za kigeni, lakini pia atakumbukwa kama mshindi wa tuzo ya Nobel na rais aliyesimamia Mkataba wa Camp David, ambao ulileta makubaliano ya amani kati ya Israeli na Misri. Jimmy Carter amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 100 siku ya Desemba 29, 2024. #bbcswahili #marekani #jimmycarter Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw