Familia yamuomboleza binti yao aliyefariki baada ya KCSE

  • | Citizen TV
    8,680 views

    Huku Familia mbalimbali zikisherehekea matokeo mazuri baada ya wana wao kutia fora kwenye mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE mwaka huu, familia moja kijijini Kiamirega katika wadi ya Ichuni kaunti ya Kisii haina tabasamu, kutokana na maafa ya mwana wao Michelle Kemunto Oguto aliyefariki baada ya kumaliza mtihani na kupata alama ya B-. Mitchell anaripotiwa kuaga dunia siku mbili tu baada ya kukamilisha mtihani wake.