Wanaoishi mpakani wa Kenya-Somalia wapewa hakikisho la usalama

  • | Citizen TV
    323 views

    Balozi wa amani nchini Somalia Ali Korane amewahakikishia wenyeji wanaoishi mpakani mwa Kenya na Somalia kuwa amani imerejea baada ya mazungumzo baina ya viongozi wa nchi hiyo. Korane amesema tayari amefanya mazungumzo na Rais pamoja na waziri mkuu wa nchi hiyo kwa nia ya kukomesha vita kati wanajeshi wa serikali kuu na wale wa Jubaland, machafuko yaliyoshuhudiwa yamewafanya wenyeji mpakani kuwa na wasiwasi na kuwasababishia hasara kubwa. Akiongea mjini Garissa, Korane amesema machafuko nchini Somalia yataongeza idadi ya wakimbizi katika kambi za Dadaab na kuleta ushindani wa raslimali kwenye eneo hilo.