Wanafunzi wa vyuo vikuu wana wasiwasi kuhusu hatma yao

  • | Citizen TV
    274 views

    Wanafunzi wanaotegemea ufadhili wa serikali katika vyuo vikuu vya humu nchini wameingia wasiwasi kuhusu malipo ya karo na pesa za matumizi baada ya mahakama kuharamisha mfumo mpya wa ufadhili. Hata hivyo wizara ya elimu inasisitiza kuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wa pili watapata ufadhili kwa wakati unaofaa kwani tayari fedha hizo zilikuwa zimekadiriwa kwenye bajeti.