Waziri wa afya na katibu wake watofautiana

  • | Citizen TV
    2,674 views

    Hali ya suitafahamu ilishuhudiwa katika afisi za wizara ya Afya baada ya aliyekuwa afisa mkuu wa KEMSA Andrew Mulwa, kuripotiwa kufika kazini kuchukua jukumu lake jipya kama mkuu wa idara ya udhibiti w amagonjwa ya zinaa na ukimwi - NASCOP - . Hii ni licha ya uteuzi wake kukomeshwa na waziri wa Afya Debrah Mulongo. Hata hivyo, Katibu wa wizara ya Afya Harry Kimtai ambaye alitekeleza uajiri huo uliosababisha aliyekuwa mkuu wa NASCOP kuelekea katika kituo cha kuangazia maslahi ya wakongwe nchini, amesema kwamba alitekeleza mabadiliko hayo kisheria.