Mbunge wa Dadaab afurushwa chamani cha Wiper kwa kukosa nidhamu

  • | Citizen TV
    1,331 views

    Mbunge wa Daadab na naibu mwenyekiti wa chama cha Wiper Farah Maalim amefurushwa kutoka kwa chama cha wiper, kwa madai ya kukosa nidhamu na kukosa kuheshimu katiba ya chama hicho. Maalim ambaye aligonga vichwa vya habari kwa kusema angewauwa waandamanaji 5,000 wa gen z kila siku kama angekuwa rais, pia aliwatusi wanaomkashifu Rais William Ruto chini ya wiki moja iliyopita.