Basari zilizotolewa na magavana zapingwa na msimamizi wa bajeti Margaret Nyakang'o

  • | Citizen TV
    1,125 views

    Maelfu ya wanafunzi wanaotegemea ufadhili wa masomo kutoka kwa serikali za kaunti huenda wakasalia kwenye njiapanda kufuatia agizo la msimamizi wa bajeti Margaret Nyakang'o kuwa hawataweza kupata fedha hizo kwa sasa. Kwa mujibu wa Nyakang'o, pesa hizo zitatolewa tu endapo kutakuwa na makubaliano na serikali kuu, kwani serikali za kaunti hazina majukumu katika shule za upili, vyuo vikuu na vyuo vya kiufundi.