Serikali ya kaunti ya Kisii yaafikia makubaliano na wauguzi

  • | KBC Video
    19 views

    Chama cha Kitaifa cha Wauguzi (KNUN), tawi la Kisii, kimesitisha mgomo wake baada ya kuafikiana kuhusu makubaliano na serikali ya kaunti. Akiwakilisha gavana wa kaunti ya Kisii, Simba Arati, naibu gavana, Charles Obebo, alitia saini mkataba wa kurejea kazini na wauguzi hao, na kuondoa hofu ya mgomo katika sekta ya afya. Naibu gavana huyo alipongeza wahudumu hao wa afya kwa kujitokeza kwa wingi kuhakikisha wagonjwa katika kaunti hiyo hawalazimishwi kusafiri kwenda maeneo mengine kutafuta huduma za matibabu. Miongoni mwa masuala yenye utata ambayo wauguzi hao waliibua ni kushindwa kwa mwajiri wao kuteua tena wauguzi maalum, kutoa bima ya afya kamili na kutekeleza muundo wa mishahara ya tume ya mishahara na marupurupu ya 2024.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive