Skip to main content
Skip to main content

Madaktari Kaunti ya Kiambu wasitisha mgomo

  • | KBC Video
    1,520 views
    Duration: 3:59
    Madaktari katika Kaunti ya Kiambu wamesitisha mgomo wao kufuatia kusainiwa kwa makubaliano kati ya serikali ya kaunti hiyo, chama cha madaktari humu nchini KMDU na baraza la magavana. Akizungumza jijini Nairobi baada ya mkutano wa mashauriano kati ya pande hizo tatu, katibu mkuu wa KMPDU, Davji Atellah, aliwasihi madaktari hao kuendelea na kazi siku ya Jumatatu wiki ijayo. Madaktari wa Kiambu wamekuwa kwenye mgomo kwa siku 150 tangu tarehe 26 mwezi Mei mwaka huu.Mwafaka uliafikiwa baada ya madaktari hao kutia saini mkataba wa kurejea kazini unaoshughulikia malalamishi yao huku kuwekwa ratiba wazi ya utekelezaji kukiwa muhimu katika kukomesha mgomo huo. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive