Tazama mubashara hafla ya uapisho wa rais mteule wa Marekani Donald Trump

  • | BBC Swahili
    0 views
    Rais mteule Donald Trump anaapishwa kuwa rais wa 47 wa Marekani, Januari 20,2023 Hafla ya uapisho itatanguliwa na maonesho ya muziki na hotuba ya ufunguzi kwenye jukwaa kuu lililopo kwenye majengo ya bunge la Marekani. Kisha itafuatiwa na kuapishwa kwa Trump na makamu wa rais JD Vance pamoja na hotuba ya kuapishwa. Kisha Trump ataingia Chumba cha Rais kutia saini hati muhimu za kuanza utawala wake mpya. Na baada ya chakula cha mchana ambacho rais atahudhuria, gwaride litaanza, kutoka majengo ya Bunge (Capitol) hadi Ikulu ya White. Matukio haya yote yanakujia mubashara kuanzia majira ya saa moja na dakika 45 usiku kwa saa za Afrika Mashariki kupitia ukurasa huu wa Youtube pamoja na mitandao ya kijamii na tovuti ya BBCSwahili. #bbcswahili #Marekani #donaldtrump Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw