Gor Mahia yaleweshwa na Tusker mbili

  • | Citizen TV
    348 views

    Mabingwa wa zamani wa ligi kuu ya taifa, Tusker FC wamerejea kileleni mwa ligi kuu baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mabingwa Gor Mahia. Baada ya sare tasa katika kipindi cha kwanza, Tusker FC ilichukua oungozi katika dakika ya 50 kupitia mshambulizi Ryan Ogam. Dakika ishirini baadaye, Gor Mahia ilisawazishakupitia nahodha Austin Odhiambo. Katika muda wa majeruhi, Tusker walipata bao la pili na la ushindi katika uwanja wa Machakos.