Magavana wanalalamikia uamuzi wa msimamizi wa bajeti nchini kuhusu basari

  • | Citizen TV
    804 views

    Magavana sasa wanamtaka msimamizi wa bajeti Margaret nyakang'o kuwasikiliza kufuatia hatua yake ya kusitisha serikali za kaunti kutoa misaada ya kifedha ya elimu kwa wanafunzi wasiojiweza kwa kuwa ni jukumu la serikali kuu. Baraza la magavana sasa likisema kuwa uamuzi huu umewaacha njia panda wanafunzi wengi.