Ujenzi wa bwawa la Thwake yaendelea kujikokota licha ya ahadi kochokocho

  • | Citizen TV
    1,013 views

    Ujenzi wa bwawa la thwake umeendelea kujikokota licha ya ahadi kochokocho na hakikisho kutoka kwa serikali kuwa mradi huo utakamilika kwa wakati na kuwafaidi wakazi wa kaunti tatu za ukambani. Inaarifiw akuwa hali hiyo imechangiwa na kucheleweshwa kwa pesa za kumlipa mwanakandarasi anayejenga bwawa hilo, ambaye anahitaji shilingi bilioni 9.2 ili kukamilisha awamu ya kwanza ya mradi huo.