Wanawake 10,000 wasajiliwa kuuza bidhaa za shanga kupitia mtandaoni

  • | Citizen TV
    123 views

    Zoezi la kuwasajili wanawake zaidi ya elfu kumi ambao wanatarajiwa kunufaika na mradi wa vituo vinne vya kuuza bidhaa za shanga kupitia mtandaoni umen’goa Nanga katika eneo la Loitokitok Kajiado kusini. Mradi huo unaoshirikisha shirika la Ushanga Inititive na KWS umeanzisha vituo hivyo karibu na mbuga za wanyapori za Amboseli, Chyulu, na Tsavo kwa lengo la kupanua soko la ushanga na kuwapa mapato wanawake ambao wanategemea shanga kukimu maisha.