Wanafunzi wa chuo cha Nairobi wafika ofisi za HELB

  • | Citizen TV
    200 views

    Baadhi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi wamevamia ofisi za bodi ya utoaji mikopo ya wanafunzi za HELB wakilalamikia kuchelewa kwa mikopo yao Wanafunzi hawa waliokita kambi nje ya jumba la Anniversary wamelalamikia kushindwa kugharamia mahitaji yao ya elimu na kibinafsi kutokana na kuchelewa kwa mikopo hii. Polisi walilazimika kushika doria kuzuia ghasia. Baadaye wawakilishi wa wanafunzi waliruhusiwa kuingia ndani ambako maafisa wa HELB waliwaahidi kuwa wangepata malipo yao kufikia mwisho wa siku ya leo.