Kamati ya bunge yapendekeza mageuzi ya idaya ya uajiri katika sekta ya Afya

  • | Citizen TV
    115 views

    Kamati ya afya katika bunge la kitaifa chini ya uenyekiti wa mbunge wa endebes Robert Pukose, imependekeza kuundwa kwa tume ya huduma ya afya ili kutatua changamoto zinazokumba sekta ya afya nchini. Mapendekezo haya yalijiri wakati wa kikao cha kamati hiyo na jopokazi la watu 20, linaloendelea kupokea maoni kuhusu namna ya kutatua changamoto za ajira na utendakazi katika sekta ya afya. Kamati hiyo itakuwa inatoa ripoti yake mwezi ujao, baada ya kuteuliwa na rais william ruto mwezi Julai mwaka jana.