Somalia: Wanajeshi waimarisha doria wakati Trump aamuru IS kushambuliwa

  • | VOA Swahili
    189 views
    Kwa takriban mwezi mmoja, Majeshi ya Ulinzi ya Puntland wameripotiwa kusonga mbele kufikia maficho ya wapiganaji wa Islamic State katika ukanda huo, huku kikiwa na mapigano makali hivi karibuni huko Turmasaale, eneo la kimkakati. Licha ya vifo kwa pande zote mbili, wanajeshi wa Puntland wamepiga hatua kubwa, wakikamata maeneo muhimu kadhaa. Siku ya Jumamosi (Februari 1) Rais wa Marekani Donald Trump alisema aliamuru mashambulizi ya kijeshi kumlenga mpangaji mkuu wa mashambulizi ya Islamic State na wengine kutoka katika jumuiya hiyo nchini Somalia. Waziri wa Ulinzi Pete Hegseth alisema mashambulizi yalifanywa katika eneo la milima ya Golis na hakuna raia aliyedhurika. Reuters haikuweza kuthibitisha maelezo hayo. Afisa mmoja wa ofisi ya rais Somalia, akitaka jina lake lisitajwe, alithibitisha mashambuliz hayo na kusema serikali ya Somalia imeipokea hatua hiyo. Marekani katika vipindi tofauti imefanya mashambulizi ya anga nchini Somalia kwa miaka kadhaa, chini ya utawala wa Warepublikan na Wademokratik. (Reuters) #somalia #is #isis #voa