Barchok atiwa nguvuni na maafisa wa EACC

  • | KBC Video
    605 views

    Gavana wa Bomet, Hillary Barchok amekamatwa na maafisa wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi-EACC kufuatia uchunguzi unaoendelea kuhusu madai ya ubadhirifu wa pesa za kaunti hiyo na mkinzano wa maslahi ambapo gavana huyo ni mshukiwa. Maafisa wa EACC walivamia makazi yake katika kaunti ya Bomet leo asubuhi na kumkamata. Kwa mujibu wa tume hiyo, Gavana huyo yuko kizuizini na anatazamiwa kuandikisha taarifa katika afisi za tume hiyo eneo la South Rift kaunti ya Nakuru. Kukamatwa kwake kunajiri miezi kadhaa baada ya wawakilishi wadi katika kaunti ya Bomet kushinikiza kukamatwa kwake kwa madai ya matumizi mabaya ya fedha za kaunti.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive