Kaunti ya Kajiado imetenga shilingi milioni-40 kama marupurupu ya wahudumu wa afya wa nyanjani.

  • | KBC Video
    21 views

    Serikali ya kaunti ya Kajiado imetenga shilingi milioni-40 kama marupurupu ya wahudumu wa afya wa nyanjani. Wahudumu hao-1,682 watakuwa wakipokea shilingi elfu mbili kila mmoja kwa mwezi. Akiongea katika mkutano na wahudumu hao, waziri wa afya katika serikali ya kaunti ya Kajiado, Eddy Kimani alisema wizara ya fedha imetenga fedha hizo katika kipindi cha kifedha cha mwaka-2024/2025. Wahudumu hao wamesema kuwa wamekuwa wakikabiliwa na wakati mgumu kujikimu kimaisha ikiwemo kugharamia matibabu yao chini ya mpango wa SHA kutokana na ukosefu wa pesa.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive