Gavana wa Bomet ahojiwa na EACC kwa saa 7

  • | Citizen TV
    1,675 views

    Gavana wa Bomet Hillary Barchok leo amehojiwa kwa zaidi ya saa saba na maafisa wa kupambana na ufisadi, baada ya kukamatwa kwa tuhuma za ufisadi. Maafisa wa tume ya EACC walifika mapema asubuhi nyumbani kwake Barchok wakimzuilia kwa tuhuma za ufisadi wa zaidi ya shilingi bilioni moja. Na kama Kamau Mwangi anavyoarifu, Gavana Barchok anachunguzwa na watu wengine 10 wakiwemo maafisa wanane wa kaunti yake.