Washikadau wana hofu kuhusu ongezeko la visa vya ukeketaji Meru

  • | Citizen TV
    204 views

    Wasiwasi umeibuka kuhusiana na ongezeko la visa vya ukeketaji kaunti ya Meru baada ya kaunti hii kuandikisha idadi ya juu ya visa vya ukeketaji nchini. Akizungumza katika hafla iliyoangazia mikakati ya kukabiliana na ukeketaji nchini, katibu wa idara ya jinsia Anne Wang'ombe alisema kuwa baadhi ya wahudumu wa afya wanashiriki ukeketaji na kutaka wahusika kuwachukulia hatua za kisheria.