'Sera ya Elimu inahitaji kuja na ufafanuzi wa kina juu ya utekelezaji'

  • | VOA Swahili
    131 views
    Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014, toleo la mwaka 2023, inalenga kutoa elimu na ujuzi kwa wanafunzi ili kuwaandaa kwa mahitaji ya sasa na ya baadaye katika soko la ajira na maisha kwa ujumla kupitia uhimizaji wa elimu ya ujuzi kuliko kutegemea taaluma pekee. Zaida Mgala aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Uwezo Tanzania linalojishughulisha na masuala ya elimu amesema licha ya sera hiyo kuja na mipango mizuri lakini bado inahitaji kuja na ufafanuzi wa kina wa namna gani mipango hiyo inaweza kutekelezeka. Ripoti ya Amri Ramadhani, VOA, Tanzania. #sera #elimu #tanzania #soko #ajira #wanafunzi #teknolojia #waalimu #diploma #voa #voaswahili