Kamati ya usalama katika kaunti ya Trans Nzoia yaandaa kikao cha vita dhidi ya pombe haramu

  • | Citizen TV
    185 views

    Kamati ya usalama ya Kaunti ya Trans Nzoia imeandaa mkutano katika eneo la Kapsirowa, eneo bunge la Cherangany, ili kuweka mikakati ya kukabiliana na tatizo la pombe haramu katika eneo hilo. Kamati hiyo inasema kuwa pombe haramu ni mojawapo ya changamoto zinazochangia utovu wa usalama na kudorora kwa maendeleo ya jamii.