Putin amwalika Trump kwenda Moscow, Russia #voaswahili #voa #habari

  • | VOA Swahili
    244 views
    Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumatano walijadili kumaliza vita nchini Ukraine, wamekubaliana kukutana katika siku zijazo na Putin amemualika Trump mjini Moscow, Kremlin ilisema. Putin alizungumza na rais aliyeko madarakani kwa mara ya mwisho Februari 2022 wakati alipozungumza kwa simu na Joe Biden muda mfupi kabla ya kuamuru majeshi yake kuingia Ukraine. Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema kuwa Putin na Trump wamejadili Mashariki ya Kati, uhusiano wa pamoja, Ukraine na mabadilishano ya wafungwa kati ya Washington na Moscow, shirika la habari la serikali TASS limeripoti . #voaswahili #afrika #putin #trump #ukraine #russia #marekani VOA Swahili inarusha matangazo ya Duniani Leo kupitia Tovuti yetu na jukwaa la Facebook Jumatatu hadi Ijumaa tukikuletea habari mbalimbali za siasa na uchambuzi kwa lugha ya Kiswahili. Tembelea tovuti yetu voaswahili.com/duniani-leo na Makala Maalum ya Jarida la Wikiendi. Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu. Matangazo yetu yanasambazwa kupitia satellite, cable, FM na MW, na and kupitia mtandao wa vituo vya matangazo vya washirika wetu takriban 3000. Tangu kuanzishwa mwaka 1942, Sauti ya Amerika imeendelea na azma yake ya kutoa habari za kina na kuwaambia wasikilizaji wake ukweli. Tangu kipindi cha Vita Vya Pili vya Dunia, Vita Baridi, Vita dhidi ya ugaidi wa kimataifa, na juhudi za ukombozi duniani kote hivi leo VOA imekuwa mfano katika kutekeleza kanuni za vyombo vya habari huru. Jiunge na VOA Swahili: » Tembelea Tovuti Yetu: https://bit.ly/3PtyNWc »Angalia Video Zaidi za VOASwahili: https://bit.ly/3TNTiiI »Pakua VOA+ katika vifaa vya Apple : https://bit.ly/VOAPlus »Download VOA+ katika vifaa vya Android https://bit.ly/3KykriI »Tembelea Tovuti yetu: https://www.voaswahili.com/ »Upende ukurasa wetu wa Facebook: https://www.facebook.com/voaswahili »Tufuatilie katika Instagram: https://www.instagram.com/voaswahili »Tufuatilie katika X: https://twitter.com/voaswahili »Tufuatilie katika YouTube: https://www.youtube.com/@VOASwahili