Kwa nini Uganda inashinikizwa kumuachilia Besigye?

  • | BBC Swahili
    2,206 views
    Shinikizo limeendelea ndani na nje ya Uganda kutaka kuachiliwa huru kwa kiongozi wa upinzani Kizza Besigye ambaye amedhoofika kiafya tangu alipoanza kususia chakula wiki iliyopita. Katika taarifa ya pamoja iliotolewa leo mjini Nairobi, mashirika ya kutetea haki za kibinaadam yametoa wito kwa mamlaka nchini Uganda kuheshimu uamuzi wa mahakama kuu na kumuachilia huru Kizza Besigye na washtakiwa wengine.