Maisha Afrika yamebadilika vipi chini ya utawala wa Trump?

  • | BBC Swahili
    2,169 views
    Leo Februari 20 Rais wa Marekani Donald Trump amekamilisha mwezi mmoja tangu alipochukua rasmi hatamu ya uongozi wa taifa hilo mwaka huu. Donald Trump ameidhinisha amri kadhaa za kiutendaji baada ya kurejea katika kiti cha uongozi wa Marekani, akiahidi kuchukua hatua za haraka katika baadhi ya ahadi alizotoa wakati wa kampeni. Amri hizo zimekuwa na athari gani barani Afrika?