Kaunti ya Murang'a imezindua kituo tamba cha matibabu ya figo

  • | Citizen TV
    286 views

    Kaunti ya Murang'a imezindua kituo tamba cha matibabu ya ugonjwa wa figo maarufu kama Renal Roads. Kituo hicho cha kipekee ni cha kwanza nchini na kinatarajiwa kuwasaidia pakubwa wagonjwa kwa kuleta matibabu karibu nao. Kituo hicho tamba cha kusafisha figo kimefanikishwa kwa ushirikiano na bena care, kaunti ya murang'a na washirika wengine. Hatua hiyo inalenga kuwapunguzia wagonjwa safari ya kutafuta matibabu katika hospitali zilizo mbali nao. Uzinduzi wa kituo hicho ulifanyika katika hospitali ya Kirwara.