Utumishi kwa wote : Wafanyakazi wa serikali Mbeere walaumiwa kwa utepetevu

  • | KBC Video
    35 views

    Mbunge wa Mbeere kaskazini, Geoffrey Ruku ameelezea kutoridhishwa na huduma duni zinazotolewa na baadhi ya maafisa wa umma. Ruku alisema kuwa wengi wa maafisa wa serikali huzingatia maslahi yao wenyewe badala ya kuhudumia umma. Alitoa wito wa kukomeshwa kwa mtindo huo akisisitiza haja ya wafanyakazi kuwajibika kuwahudumia wakenya. Akiongea katika kanisa katoliki la St. James huko Gitiburi, Mbeere kaskazini, kaunti ya Embu , Ruku alitoa wito kwa mkuu wa utumishi wa umma Felix Kosgey, kuhakikisha kuwa watumishi wa umma wanawajibikia majukumu yao.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive