Wagonjwa walazimika kulipa pesa taslimu baada ya hspitali kususia SHA

  • | Citizen TV
    412 views

    Shughuli za matibabu katika hospitali kadhaa zilitatizika huku sehemu za kupokea wagonjwa katika baadhi ya hospitali zikisalia bila watu kufuatia kusitishwa kwa huduma za SHA katika hospitali za kibinafsi. Wagonjwa wamelazimika kulipa pesa taslimu huku jamaa zao wakiagizwa kuwahamisha wale ambao hawana pesa. Muungano wa hospitali za kibinafsi (KAPH), ule wa hospitali za kibinafsi za mashinani na mijini (RUPHA) ambazo zinajumuisha zaidi ya hospitali elfu moja sasa zimesusia huduma za SHA hadi serikali iwalipe madeni inayodaiwa.