Sudan kuzuia ndege za Kenya, katika Dira ya Dunia TV

  • | BBC Swahili
    6,140 views
    Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Sudan amesema huenda taifa hilo likapiga marufuku ndege za Kenya kutumia anga yake, pamoja na kusitisha kuagiza majani chai baada ya serikali ya Kenya kuruhusu kikosi cha Rapid Support Forces (RSF) na washirika wake kutia saini hati ya serikali mbadala. Katika mahojiano ya kipekee na BBC, Ali Youssef ameilimbikizia Kenya lawama pamoja na Umoja wa Milki za Kiarabu UAE kwa kuwezesha mkutano huo kufanyika.