Wito watolewa kuwe na mikakati ya kuwezesha wanawake

  • | KBC Video
    3 views

    Wadau katika sekta ya uchumi wanatoa wito wa kutekeleza mikakati ya kuwasaidia wanawake wajasiriamali. Akizungumza katika kongamano la kila mwaka la kiuchumi la kina mama humu nchini, mwenyekiti wa mpango wa kutetea na kuhamasisha jamii, Daisy Amdany alisisitiza kuwa licha ya wanawake kumiliki asilimia-43.1 ya biashara ndogo na za kadri, wengi wao wanakabiliwa na changamoto si haba. zikiwemo uhaba wa fedha, ukosefu wa maarifa ya kifedha na tatizo la kutolipwa kikamilifu na hivyo kuathiri ustawi wao wa kiuchumi. Wataalamu katika kongamano hilo walisisitiza haja ya kuimarisha upatikanaji wa fedha, mfumo dhabiti wa kisheria na usawa wa kijinsia pamoja na kuboreshwa kwa elimu kuhusu ujasiriamali ili kuwezesha wanawake kutambua kutumia kamili wao wa kiuchumi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive