Wanafunzi waeleza kinacho sababisha matumizi ya mihadharati

  • | VOA Swahili
    108 views
    Matumizi ya dawa za kulevya kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Kenya yameongezeka mpaka asilimia 45.6 kwa mujibu wa ripoti ya mamlaka ya taifa ya kampeni dhidi ya matumizi mabaya ya pombe na dawa za kulevya. Ripoti hiyo inaashiria pia ongezeko la matumizi hayo kwa wanafunzi wa kike. Wanafunzi wa kike wa vyuo vikuu wanaonyesha kiwango cha juu cha magonjwa ya unyogovu wa wastani na kali kwa asilimia 6.4 na 4.1 mtawalia ikilinganishwa na wenzao wa kiume kwa asilimia 5.2 na asilimia 3.0. Ripoti ya Zainab Said wa VOA, Nairobi, Kenya. #uraibu #mihadharati #dawazakulevya #wanafunzi #kenya #vyuovikuu #wanawake #wasichana #voa #voaswahili