Maelfu ya watu wakusanyika miji mbalimbali kushinikiza haki ifanyike

  • | VOA Swahili
    71 views
    Maelfu ya watu wamekusanyika katika miji mbalimbali kote Ugiriki Ijumaa kushinikiza haki ifanyike katika maadhimisho ya pili ya ajali mbaya ya treni kuwahi kutokea, huku wafanyakazi katika sekta ya usafiri wa ndege, majini na treni wakigoma. Watu 57 walifariki wakati treni ya abiria iliyokuwa imejaa wanafunzi ilipogongana na treni ya mizigo Februari 28, 2023, karibu na Tempi gorge huko katikati ya Ugiriki Miaka miwili baadaye, mianya ya usalama ambayo ilisababisha ajali hiyo haijatatuliwa, uchunguzi ulionyesha hivyo Alhamisi. Uchunguzi wa kujitegemea wa mahakama bado haujakamilika, na hakuna aliyehukumiwa katika ajali hiyo. Maandamano ya umma yalikuwa yamepangwa kufanyika katika darzeni ya miji kote nchini. Safari zote za ndege za ndani na za kimataifa zilisitishwa wakati waongoza ndege wakiungana na waendesha feri, treni, madaktari, mawakili na waalimu katika mgomo wa jumla wa saa 24 kuwaenzi waathirika wa ajali hiyo. Biashara zilifungwa na majumba ya burudani yalifuta maonyesho. Hadi kufikia asubuhi, maelfu walikuwa wamekusanyika katika Bustani ya Syntagma katikati ya Athens, huku wakisimamiwa na askari wa kuzuia ghasia. Bango moja lilisoma: “Serikali ni wauaji.” Serikali ya mrengo wa kati-kulia ya Waziri Mkuu Kyriakos Mitsotakis ambayo ilishinda tena uchaguzi baada ya ajali ya mwaka 2023, imekabiliwa na ukosoaji mara tena kutoka kwa ndugu wa wahanga kwa kushindwa kuanzisha uchunguzi wa bunge ikiwa ni kuwajibika kisiasa. Serikali imekanusha kufanya makosa yoyote na kusema ni juu ya mahakama kuchunguza ajali hiyo. - Reuters #athens #ugiriki #ajali #treni #mahakama #mgomo #wafanyakazi #ndege #majini #treni