Kumwezesha mtoto wa kike : Shule ya kutwa ya wasichana kujengwa Narok

  • | KBC Video
    7 views

    Serikali ya kaunti ya Narok imetenga shilingi milioni-15.8 kugharamia ujenzi wa shule ya umma ya wasichana ya Kiislamu katika kaunti hiyo. Shule hiyo ya kutwa itakuwa shule ya kwanza ya aina yake katika kaunti hiyo. Akiongea wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa madarasa, mwenyekiti wa chama cha maslahi ya Waislamu katika kaunti ya Narok Mahmud Hassan Yunis alisema shule hiyo itawapokea wanafunzi wa dini mbali mbali. Ujenzi wa shule hiyo utakamilika katika kipindi cha miezi sita.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive