Chanzo cha ugonjwa usioeleweka katika eneo la Tabaka kaunti ya kisii ni maji wanayotumia

  • | K24 Video
    96 views

    Kufuatia kuzuka kwa ugonjwa usioeleweka katika eneo la tabaka kaunti ya kisii, katibu wa wizara ya afya ya umma, Mary Muthoni sasa ametaja chanzo cha ugonjwa huo kuwa ni maji wanayotumia. Akihutubia wakazi katika eneo la Amarondo, Muthoni amewataka wakazi wakome kutumia maji kutoka mtoni, akisema matokeo ya awali ya uchunguzi wa maabara yalionyesha maji hayo sio safi. Inasemekana maji yanayotumiwa yamechanganyikana na kinyesi.