Kamati ya Seneti yamtetea mkaguzi mkuu wa mahesabu serikalini

  • | K24 Video
    20 views

    Kamati ya bunge la seneti ya uhasibu wa mali ya umma leo imemtetea mkaguzi mkuu wa mahesabu serikalini daktari Nancy Gathungu. Gathungu alikuwa amefika mbele ya kamati hiyo kutetea ripoti yake iliyotilia shaka mfumo wa sha na kuibua mjadala nchini. Maseneta wakiongozwa na seneta wa Nairobi Edwin Sifuna wametaka kuheshimiwa kwa taasisi zinazochunguza utendakazi wa serikali. Hili linakuja huku ripoti zikiashiria kuwa kuna mswada ambao umewasilishwa bungeni ili kupunguza mamlaka ya afisi ya mkaguzi mkuu.