Wakazi wa maeneo ya Majengo na Pumwani waandamana baada ya kijana wa miaka 17 kuawa

  • | K24 Video
    1,634 views

    Baadhi ya wakazi wa maeneo ya Majengo na Pumwani jijini Nairobi waliandamana asubuhi kufuatia kuuawa kwa risasi kwa kijana wa miaka 17 katika operesheni ya polisi. Vijana wawili walifariki ikiwemo kijana wa miaka 17 ambaye alipigwa risasi kichwani huku mwingine kupigwa risasi mguuni na kufariki baada ya kufikishwa hospitalini. Maandamano hayo yalivuruga biashara baada ya magari mawili ya polisi kuchomwa na barabara kufungwa. Hii imepelekea kifo cha kijana mmoja katika vuta nikuvute hiyo ikijumuisha idadi ya vijana watatu kufariki. Hata hivyo familia ya marehemu imelilia haki ya mwanao Ibrahim Chege katika makafani ya hospitali ya kenyatta hii leo.