Vyuo vikuu viko hatarini kufungwa kufuatia mgogoro wa kifedha wa shilingi bilioni 13.7

  • | K24 Video
    44 views

    Vyuo vikuu vitafungwa ifikapo mwisho wa mwaka huu wa fedha ikiwa serikali itashindwa kulipa mikopo inayofikia shilingi bilioni 13.7. Kulingana na katibu mkuu wa elimu ya juu, Beatrice Inyangala, hali inazidi kuwa mbaya kutokana na upungufu wa shilingi bilioni 11.2 kwa ajili ya ufadhili wa masomo. Mgogoro huu wa kifedha unatokea wakati katibu mkuu wa elimu ya msingi, Belio Kipsang, alikiri kuwa serikali haiwezi kulipa madeni yaliyobaki, pindi mwaka wa fedha unapomalizika, hadi sasa ni 25% tu ya ufadhili uliowasilisha kwa muhula wa kwanza