Viongozi waliohudhuria hafla ya ushirikiano kati ya UDA na ODM waipongeza hatua hiyo

  • | K24 Video
    125 views

    Viongozi waliohudhuria hafla ya kutiwa saini mkataba wa ushirikiano kati ya chama cha UDA na chama cha ODM wameipongeza hatua hiyo, wakiitaja kama hatua ya kijasiri ya kulihakikishia taifa umoja na maendeleo. akiongozwa na naibu rais Kithure Kindiki,viongozi hao wameweka wazi matumaini kuwa hatimaye changamoto zinazokumba taifa kama vile kupanda kwa gharama ya maisha, uhaba wa ajira kwa vijana na ufisadi zitatatuliwa kufuatia ushirikiano huo.