Asilimia 45 ya wanawake wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 49 wakumbwa na ukatili wa kijinsia

  • | K24 Video
    77 views

    Angalau asilimia 45 ya wanawake wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 49 wamekumbwa na ukatili wa kijinsia. Wizara ya afya sasa inakadiria kuwa ni asilimia 14 pekee ya visa hivyo vinavyoripotiwa. Huku dunia ikiadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake, serikali imeshinikizwa kuimarisha sera na mifumo ya msaada kwa waathiriwa. katika juhudi za kukabiliana na janga hili, kituo maalum cha kuwahifadhi waathiriwa wa ukatili wa kijinsia kimezinduliwa jijini Nairobi. kituo hicho kitatoa huduma za afya, na mafunzo ya ujuzi zaidi dhidi ya ukatili wa kijinsia na msaada wa kisaikolojia