Mkataba kati ya Ruto na Raila waendelea kuibua hisia mseto

  • | KBC Video
    3,854 views

    Mkataba wa ushirikiano wa kikazi baina ya chama cha UDA na kile cha ODM uliotiwa saini siku ya Ijumaa na rais William Ruto na aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga, unaendelea kuibua hisia mseto hapa nchini. Huko Kilifi, gavana Gideon Mung’aro alisema ushirikiano huo utawezesha utekelezaji wa ripoti ya kamati ya mazungumzo ya kitaifa-NADCO. Haya yanajiri huku kundi la viongozi wa makanisa kutoka eneo la Ukambani, likitoa wito wa umoja wa jamii ya wakamba, na kuunga mkono azma ya kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka, ya kuwania urais mwaka 2027.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive