Waziri wa utumishi wa umma Justin Muturi asema hatajiuzulu

  • | Citizen TV
    1,268 views

    Waziri wa utumishi wa umma Justin Muturi amepuuzilia mbali shinikizo za wandani wa Rais William Ruto wakimtaka ajiuzulu. Waziri Muturi akizungumza kwenye kipindi cha JKL cha Runinga ya Citizen amepuuza tetesi kuwa huenda akajiuzulu karibuni akisema bado yuko ndani ya serikali. Aidha ametetea msimamo wake kwa serikali kuhusu kutekwa nyara kwa vijana