Washukiwa wanane wa wizi Thika road wakamatwa

  • | Citizen TV
    1,022 views

    Idara ya upelelezi wa jinai DCI imesema imewakamata washukiwa wanane wanaodaiwa kuhusika na wizi ulioshuhudiwa katika barabara ya Thika baada ya ziara ya rais William Ruto. Washukiwa hao wanadaiwa kuwa miongoni mwa makundi ya vijana waliokuwa wanavamia watu pamoja na maduka na pia kuwaibia wenye magari katika barabara ya Thika.